Wauza ‘unga’ kuminywa kibububu.

 Katika kubadili mtindo wa kushughulikia wauzaji, watumiaji, wazalishaji na wasafirisha wa dawa za kulevya, Serikali imeamua kuendesha kimyakimya vita hiyo kimyakimya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Kupambana na Dawa za Kulevya, alisema jana kuwa iwapo watagundua mhusika hana hatia ataachiwa huru.
Alitoa kauli hiyo alipofungua kongamano la mmomonyoko wa maadili na athari za dawa za kulevya, lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na waumini wa Kiislamu, maaskofu, makamishna wa mamlaka ya dawa za kulevya, Jeshi la Polisi, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Dawa za Kulevya, Rogers Sianga na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk Anna Peter Makakala.
Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Abubakar Zuberi alisema nchi imekosa mwelekeo katika maadili. “Lazima lipatikane kundi la kukemea mabaya, tuwachunge waumini wetu katika maadili mema,” alisema.
chanzo:mwananchi.

Comments