Watu wenye ulemavu wameiyomba serikali kuzisimamia kwa umakini kesi zao.

ulemavuWatu wenye ulemavu wameiyomba serikali  kuzisimamia kwa umakini kesi zinazofikishwa Mahakamani ambazo zinawakabili kwani baadhi hazifikii mwisho katika kupatiwa maamuzi  nakupelekea  kukosa haki zao.

Sabra Zubeir Makame na Halima Juma Ali wamesema watu wenye ulemavu wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya udhalilishaji na kesi inapofikishwa mahakamani  hukosekana ushahidi  kutokana na  hushindwa kujielezea kulingana na ulemavu wao.


Akijibu malalamniko hayo Mrajis wa Mahakama kuu Zanzibar George Kazi amesema kesi za watu wenye ulemavu zimekuwa zikisikilizwa kwa umakini zinapofikishwa mahakaman ili kila mmoja haki yake iweze kupatikana.

Aidha George ametoa wito kwa jamii iwapo wanakesi ambazo hazijapatiwa ufumbuzi hasa za watu wenye ulemavu kwenda mahakamani kutoa taarifa ili kupatiwa haki zao na watuhumiwa wa kesi kuweza kuchukuliwa hatua za kisheria.
chanzo: Zanzibar24.

Comments