
Ajali hiyo iliyohusisha basi la kubeba abiria na lori la
kusafirisha mafuta ghafi ya kupikia ilitokea katika eneo la Kambu,
karibu na Mtito Andei.
Mkuu wa polisi wa eneo la Kibwezi Leonard
Kimaiyo ameambia BBC kuwa watu 23 walifariki papo hapo na mwingine mmoja
akafariki akitibiwa hospitalini.
Watu 20 walipata majeraha na kupelekwa katika hospitali za miji ya Kibwezi na Makindu.
Bw
Kimaiyo amesema walionusurika waliambia maafisa wa polisi dereva wa
basi alikuwa akijaribu kupita gari jingine basi lilipogongana na lori
hilo.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Taifa ya Uchukuzi Kenya, watu 3,000 hufariki kila mwaka kutokana an ajali za barabarani.
chanzo:Bbc.
Comments