Wanne wapigwa faini na kupelekwa chuo cha mafunzo baada ya kuzidi kwenye gari ya abiria.

Watu wanne (4) wapigwa faini ya elftano (5000) kila mmoja na kutumikia  chuo cha mafunzo muda wa mwezi mmoja kwa kosa la kuzidi ndani ya gari ya abiria jambo ambalo ni kosa kisheria.
Washtakiwa waliopewa hukumu hiyo ni Ame Hassan Ame (27) mkaazi wa Pita na Zako,  Heri nyambuto nyangata (25) makaazi wa kijichi, Fidha  Mohd Said (21) mkaazi wa kijichi na  John Ilyas Moris (35) mkaazi wa Bububu.

Imedaiwa mahakamani hapo na muendesha mashtaka wa polisi Sajent Hassan Mussa Mshamba mbele ya hakimu  Nassir Faki Mfaume kuwa siku ya tarehe 3 mwezi wa 4 majira ya saa moja asubuhi huko kujjichi bila ya halali wamepatikana wakiwa wamezidi ndani ya Gari yenye namba za usajili Z956  AWW yenye ruti namba  120 ikitokea upande wa Bububu Polisi na kuelekea Mndo jambo ambalo ni kosa kisheria.
Baada ya kusomewa kosa hilo washtakiwa walikiri bila ya kuwa na shaka lolote ndipo walipopewa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwao na wengine wenye tabia kama hiyo.
chanzo:zanzibar24.

Comments