Wamesema ule utamaduni wa zamani kuwa wanaume ndio kila kitu,
umepitwa na wakati na kwa karne hii, lazima wanawake wajitokezea na
kujibebesha ujemedari wa kufanya uamuzi.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wanawake hao wajasiriamali,
walisema utamaduni wa miaka 30 nyuma kuwa waanume ndio kila kitu hasa
kwenye uamuzi, sasa haupo tena.
Mwenyekiti wa ushirika wa upandaji migomba ‘tumeamua ‘shehia ya Kiuyu
kigongoni wilaya ya Wete Pemba, Fatma Said Juma, alisema sasa wanawake
lazima wathubutu kuendesha vikao na kutoa uamuzi.
Alisema haipendezi na wala haingii akili, kuona wanawake wanashindwa
kufanya vikao mbali mbali vikiwemo vya harusi, uamuzi wa kumsomesha
mtoto, vikao vya asasi vya kiarai pasi na kuwepo wanaume.
Mwenyekiti huyo alieleza kuwa, sasa wanawake wameshaelimika na kupata
ujasiri kwa kufanya shughuli zao mbali mbali za maendeleo, hivyo
wasishindwe na kuendesha vikao na mikutano yao.
“Inawezekana wazazi na walezi wetu, sisi wanawake walitunyima haki
yetu ya kushiriki na kushirikishwa kwenye vikao mbali mbali, kwa dhana
kwamba hatuwezi, lakini sio sahihi’’,alilamika.
Kwa upande wake Mwemyekiti wa Jumuia ya Kuhifadhi Mazingira Vitongoji
VECA wilaya ya Chakechake Sifuni Ali Haji, alisema wanawame wanauwezo
mkubwa na kupelekea maendeleo makubwa.
“Mimi ni mwenyekiti wa VECA mbona tumeshapata miradi miengi, ingawa
kuwa kushirikiana na wenzangu, lakini wenyewe tumekuwa watundu wa
kuendesha vikao vyetu.
Alieleza kuwa, uwezo waliojaaliwa na Muumba wa kufanya kazi na kutoa
uamuzi, laiti kama hata hao wazazi waliopita wengewashirikisha vya
kutosha, leo hii kusingekuwa na wanamke anaelilia kuporwa haki yake.
Nae mwanaharakati wa maendeleo ya wanawake kisiwani Pemba Nassra
Salum Khamis, alisema baada ya wanawake kujitumbukiza kwenye
ujasiriamali na kujipatia maendeleao, hawana sababu ya kushindwa ya
kuendesha mambo mengine.
Alifahamisha kuwa, wanawake wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya
familia na hata serikali kuu, hivyo lazima nafasi yao hiyo, wasiiache na
kuona kuwa wanaume wanaweza kila kitu.
“Yapo mambo ya asili yake lazima wanaume wawe juu, mfano wa mirathi,
lakini hakuna ulazima wala sheria kuwa, vikao na mikutano mbali mbali
kwamba wanaume ndio wawe wasemaji wa kuu na waamuzi’’,alifafanua.
Nae Maulid Saleh Hamad wa Kiuyu Jimbo la Kojani, alisema wapo
wanawake waanaoendesha familia zao, kutokana na kuamua kujiingiza kwenye
ujasiriamali, na kupata mafanikio.
“Sasa wanawake lazima tuachane na utamaduni wa zamani kwamba kila
kikao na kila jambo eti wasubiriwe wanaume, na kama hawakuja kivunjike,
hili sasa sio sahihi”,alifafanua.
Hata hivyo hivyo Mwenyekiti wa ushirika wa wasusi wa mikoba na
utengenezaji sabuni wa “subira njema” uliopo Changaweni Mkoani, Amina
Said alieleza kuwa, usawa kwenye kujiinua kiuchumi, uko sawa baina ya
jinsia mbili.
Hata hivyo Mratibu wa TAMWA Zanzibar Mzuri Issa Ali, aliwataka
wanawake wasikubali kutafutiwa haki na uamuzi na wanaume, bali sasa
wasimame wenyewe.
“Sisi tumeshwapa taaluma ya kujielewa na kujiendeleza kiuchumi, sasa
kama wameona kuwa wanauwezo wa kujiendeleza, ndio tunakotaka kwenda
huko, kila mmoja asimame mwenyewe’’,alifafanua.
Kwa upande wake Hassan Haji Khamis mkaazi wa Machomane Chakechake,
alisema wanawake wakiendelea kupewa elimu na nyenzo za kujiletea
maendeleo, wanaweza kujihudumia wenyewe.
“Inawezekana hapo zamani wanawake walikuwa hawajapata taaluma na
kujielewa kuwa wanahaki sawa kwenye kutoa uamuzi au kuitisha vikao, pasi
na kusubiri wanaume’’,alifafanua.
Hata hivyo mwanasheria Mohamed Hassan Ali, wakati akiwasilisha mada
kwa vikundi vya wanawake wa mkoa wa kaskazini Pemba, alisema maendeleo
hayamsubiri mwanamke eti mpaka ashirikishwe kwenye uamuzi na wanaume.
“Mwanamke na mwanamme wako sawa, wote wanaweza kuwa viongozi na
kuongoza vikao, na kisha kufanya uamuzi pasi mmoja kumsubiri
mwenzake’’,alifafanua.
Katika miaka ya hivi karibuni kundi la wanawake hapa Tanzania na
visiwani, wamekuwa wakijitokeza kwenye shughuli mbali mbali za
kujieletea maendeleo, ambapo zaidi ya asilimia 35 ya wanawake ni
wafanyabiashara ndogo ndogo.
chanzo: zanzibar24.
Comments