
Punde tu mpango huo utakapo kamilika, hatua hiyo itamaliza ghasia za
miongo kadhaa zilizosababisha vifo vya wau zaidi ya 800 na kujeruhiwa
kwa maelfu wengine katika kampeni kali ya kundi la ETA katika kupigania
uhuru wa Basque katika maeneo ya Uhispania na Ufaransa.
Na iwapo
ETA itasalimisha silaha zake itakuwa ndio mwisho wa uasi Ulaya. Kundi
hilo linatarajiwa kuvunjika katika miezi inayokuja.
Kwa miongo kadhaa, kundi la ETA lilihusishwana
milipuko, mauaji na uporaji. Kwa wafuasi wake ilikuwa ni kupigani uhuru
wa Basque, kwa waathiriwa wa ghasia zake, umekuwa muda wa uoga mwingi na
kupoteza wapendwa.
Leo eneo la Basque huko Uhispania ni tofuati.
Hakujashuhudiwa mashambulio kwamiaka kadhaa na ETA lilitangaza hatua ya
kusalimisha silaha mnamo mwaka 2011. Lakini imechukua wakati wote huu
kuwashawishi wafuasi wake kufanya hivyo, na kujaribu kusaka silaha
zilizosalia.
Taarifa ya ETA hatahivyo inaonya kuwa wale inaowataja
kuwa maadui wa amani huenda wakaizuia hatua yao.

chanzo:Bbc.
Comments