Wamachinga walalamika kuharibiwa mali zao baada ya vibanda vyao kubomolewa.

Vibanda vilivyopo pembezoni mwa Jengo la Machinga Complex Ilala jijini Dar es salaam vimebomolewa na  Wafanyabiashara hao walalamika kuharibiwa vibaya kwa mali zao.
Wafanyabiashara hao kwa masikitiko zaidi wanasema kubomolewa vibanda vyao vya biashara na uharibifu wa Mali zao ni uonevu na wao hawana la kufanya.

Kuna taarifa nyengine zinasema kuwa wafanyabiashara hao walipewa taarifa ya kuhama sehemu hiyo na wabomoe vibanda vyao na wahamie ndani ya Jengo hilo la Dar es salaam Business Park, au Machinga Complex.
Wafanyabiashara wamewasha moto katikati ya barabara nje ya jengo hilo kama ishara ya kukasirishwa na uvunjwaji wa vibanda vyao.
chanzo:zanzibar24.

Comments