Wakaazi wa Chaani waiyomba serikali kuwatengezea barabara ili waweze kuondokana na matatizo yayowakabili.

Wakizungumza na Zanzibar24 Wakaazi hao na madereva wa njia hiyo
wamesema kwa kipindi kirefu wamekabiliwa na tatizo hilo bila kupatia
ufumbuzi jambao linalosababisha kuzorota kwa maendeleo kijijini hapo.
Hata hivyo wamesema mara kwa mara wamekuwa wakiwatumia viongozi wao
wa jimbo kuwaombea katika serikali juu ya kujengwa kwa barabara hiyo
lakini mpaka sasa hawajaona matumaini ya kujengwa kwa njia hiyo.
Aidha wamesema pindipo serikali itakuwa msatari wa mbele katika
kuijenga njia hiyo itwasaidi vijana kuondokana na tatizo la ukosefu wa
ajira linalosababishwa na ubovu wa Barabara kutokana na kushindwa
kusafirisha biadhaa mbalimbali wanazo zalisha ikiwemo bidhaa za kilimo
kupeleka katika masoko.
wakikabiliwa na tatizo la ubovu wa barabara bila ya kupatiwa ufumbuzi.
chanzo: Zanzibar24.
Comments