Wafuasi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria wakiwa pamoja na wanafunzi na wanachuo wa taasisi mbali mbali za elimu nchini humo, waliandamana kwa amani na kisha kupiga kambi nje ya manjengo ya Bunge katika mji mkuu Abuja, ambapo wamekabidhi waraka wa matakwa yao kwa afisa mmoja wa Bunge.
Waandamanaji hao wamesema kuwa harakati hiyo ni ya amani na haina historia ya kutumia mabavu wala silaha. Wamesema Sheikh Zakzaky amekuwa akihubiri amani kwa zaidi ya miongo mitatu na hivyo tuhuma dhidi yake eti anachochea ghasia nchini humo hazina msingi.
Licha ya muhula uliotolewa na Mahakama ya Federali kwa ajili ya kuachiliwa huru msomi na mwanaharakati huyo wa kidini kumalizika tarehe 16 Januari mwaka huu, lakini serikali haijatekeleza amri hiyo.
Kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa tarehe Pili Disemba mwaka jana na mahakama hiyo, kitendo cha kuendelea kushikiliwa na serikali ya nchi hiyo Sheikh Zakzaky, mke na wanaharakati wengine wa Kishia ni kinyume cha sheria.
chanzo:parstoday.
Comments