
Akizungumza na wafuygaji wa samaki huko katika ukumbi wa mikutano
weni , amesema ni vyema kwa wafugaji wa samaki kuyatimia mabwawa hayo kwa ajili
kuongeza uzalishaji ambao utawasaidia kimaisha.
Amesema wafugaji wa samaki wamekuwa na tabia ya kuyatymia mabwawa
kwa kuombea misaada kwa wafadhili jambo ambalo halileti pia nzuri .
Akiwasilisha taarifa ya hali halisi ya ufugaji wa samaki , afisa
ufugaji wa mazao ya baharini Pemba Mohammed Salimu Othman amesema ufugaji wa
samaki umeshuka kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo wizi pamoja na ukosefu
wa vifaranga .
Mapema akifungua mkutano huo , afisa mkuu wa Idara ya maendeleo ya
uvuvi pemba , Ndg Sharif Mohammed Faki amewataka wafugaji kuweka mazimngira ya
mabwawa yao katika hali ya usafi ili kukidhi vigezo vinavyohitajika wakati huu
ambapo serikali inajiandaa kutoa vifaranga vya samaki kwa wafugaji .
Comments