
Akizungumza na Mwandishi wa Zanzibar24 huko Ofisini kwake amewataka wafanyabiasha kuhakikisha biashara zao zipo katika maeneo salama ilikulinda afya za walaji na kufata masharti ya afya.
Hata hivyo amesema maradhi ya miripuko Zanzibar bado yapo na kuna maeneo hatarishi ikiwemo Chumbuni, Daraja bovu, Bweleo, Fumba, Matemwe, Kiwengwa, Upenja hadi Kilombero na upande wapemba ni Kojani,Wete,Chake vitongoji na Michezani wananchi wachukue tahadhari sana kwa kuzidisha usafi katika maeneo yao na kuchemsha maji ya kunywa pamoja na kunawa mikono kabla ya kula.
Amesema sababu kubwa ya maradhi ya kipindupindu kujitokeza mara kwa mara nipale wananchi wanapokosa maji katika maeneo yao na kupelekea kutumia maji ya vidimbwi pamoja na uchafuzi wa mazingira.
Chanzo:Zanzibar24
Comments