Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru), Valentino Mlowola aliyasema hayo mjini hapa kwenye semina ya
Mtandao wa Wabunge wa Afrika Wanaopambana na Rushwa (APNAC) tawi la
Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu huyo alisema waandaamizi hao wanatafikishwa mahakamani kutokana na makosa ya rushwa yanayowakabili.
Alisema viongozi hao, watafikishwa mahakamani baada ya kugundulika
kushirikiana na wafanyabiashara wajanja wachache kuiibia serikali na
kulikosesha taifa mapato.
“Viongozi hawa watafikishwa mahakamani baada ya kubainika
kushirikiana na mshitakiwa mmoja aliyopo mahakamani kwa sasa kujipatia
Sh milioni saba kila baada dakika…huyo mshitakiwa hakuweza kufanya wizi
huo pekee yake, lazima alishirikiana na viongozi wa TRA maana ‘link’ ya
wizi wa mtambo wake wa kutoa stakabadhi uliunganishwa na ule wa
serikali,” alisema.
Hata hivyo, alisema Polisi wamekuwa magwiji wakubwa wa kupokea
rushwa, hivyo kuonekana kuwapo na mifumo dhaifu ya kuweza kukabiliana na
tatizo hilo.
“Kila sehemu kuna rushwa, kuanzia suala la ugaidi ambapo watuhumiwa
hupitisha silaha zao mipakani na kuwapa rushwa wahusika, dawa za kulevya
wanatoa nchi za mbali na kufikishwa nchini…kila sehemu tatizo ni hilo,”
alisema.
Vilevile, alisema tatizo la rushwa nchini bado kubwa, hivyo wabunge
wanatakiwa kushirikiana na serikali kuhakikisha wanalipigia kelele kila
wanapokuwa katika maeneo yao ya kuwatumikia wananchi.
Aidha, alisema lazima Rais awe na dhamira mahususi ya kupambana na
rushwa kama anavyofanya sasa pamoja na utawala bora ili kuweza kusaidia
kukabiliana na tatizo hilo.
Mwenyekiti wa mtandao huo, George Mkuchika alisema nchi ambayo Bunge linasumbuliwa na tatizo la rushwa haiwezi kupata maendeleo.
Mkuchika alisema nchi nyingi duniani, taasisi za usalama, mahakama na
watu wa manunuzi wamekuwa wakituhumiwa kwa rushwa kutokana na
malalamiko ya mara kwa mara, hivyo lazima tatizo hilo lipigwe vita.
Awali akifungua semina hiyo, Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema
atahakikisha ofisi yake inawahimiza wabunge katika majimbo yao,
kushirikiana na asasi zinazopambana na rushwa ili kupiga vita tatizo
hilo.
Ndugai alisema lazima wabunge washirikiane na wale ambao si wanachama
wa APNAC na wengine wa mabunge ya Afrika Mashariki kuhakikisha
wanapambana na rushwa.
chanzo:Habarileo.
Comments