Vijana wa kikundi cha Nguvu moja wameyomba serikali kuwapatia elimu ya ufugaji samaki.

Vijana wa kikundi cha Nguvu moja tusharizi wanaojishighulisha na Ufugaji Samaki huko kitogani wameiomba Wizara husika kuwaandalia mazingira maalumu ya kuwapati elimu ya ufugaji samaki ili waweze kuzalisha samaki wanaoendana na soko la ajira.
Wakizungumza na Zanzibar24 vijana hao wamesema kutokana na uhaba wa ajira uliopo katika serikali wameamua kujikita na ufugaji samaki lakini wanashindwa kufikia malengo kutoka na kukosa elimu hali inayopelekea kushindwa kuzalisha samaki wa aina mbalimbali.
Hata hivyo wamesema mbali na kuchukua jitihada ya kupeleka barua sehemu husika juu ya kuomba kusaidiwa nyenzo muhimu na Elimu ufugaji lakini bado msaada wa serikali haujafikia ipasavyo.

Aidha wametowa wito kwa vijana wenzao kuondokana na dhana ya kusubiri ajijra kutoka serikalini badala yake wazitumie fursa walizonazo katika jamii juu ya kubuni miradi ya maendeleo itakayowasaidia kujikwamua na
hali ngumu ya maisha.




Chanzo:Zanzibar24.

Comments