Kwa mujibu wa Ofisa Mifugo na Uvuvi katika Halmashauri ya Mji wa
Bunda, Rick Kaduri, tukio hilo limetokea Aprili 3 saa tisa mchana katika
kitongoji hicho wakati ng’ombe hao wakichungwa na watoto wadogo.
Kaduri alisema ng’ombe waliokufa ni mali Mwita Masero mkazi wa kijiji
cha Tairo katika Halmashauri ya Mji wa Bunda na thamani yake ni zaidi
ya Sh milioni tisa.
Alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mifugo hiyo imekufa
kutokana na kula majani ambayo kiuhalisia huwa yana sumu kali, ambapo
mifugo ikiyala kwa wingi hasa yanapoanza kuota upata madhara ya mfumo wa
chakula tumboni na hatimaye kufa.
Aidha, Kaduri alitoa mwito kwa wananchi kufukia mizoga ya mifugo hiyo
na kutokuthubutu kujaribu kula nyama ya ng’ombe wanaokufa ghafla.
Hata hivyo, alisema wamechukua sapuri ya vipimo ambavyo vitapelekwa
kwa wataalamu wa mifugo na kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi
zaidi juu ya vifo vya ng’ombe hao.
chanzo:Habarileo.
Comments