
Maafisa wa Marekani walisema kuwa waliilipua kambi hiyo kwani
ndiyo iliyotumika kuendeleza shambulizi liliotumia silaha za kemikali
yenye sumu katika mji unaodhibitiwa na waasi, ambapo watu kadhaa
walipoteza maisha siku ya Jumanne.
Lakini Urusi inaunga mkono serikali ya Rais Bashar al-Assad na imekashifu shambulizi hilo ambalo linadaiwa kuua watu sita.
Shambulio hilo linajiri siku chache tu baada ya shambulio la
gesi ya sumu lililolengwa katika mji wa Khan Sheikhoun, mkoa wa Idlib
liloua zaidi ya watu 80, wengi wao wakiwa watoto.
Upinzani wa Syria unasema kuwa ni serikali ya Syria iliyotekeleza shambulio hilo lakini serikali ya Assad inapinga haya.
Inadaiwa kuwa sasa Urusi inaweza kufanya uamuzi wa kuboresha mtindo wa Syria wa kulipua makombora.
Kwa
muda mrefu Syria ilikuwa na mfumo ulio fana sana wa ulinzi wa anga zake
lakini vita ambavyo vimekuwa vikiendelea umeudhoofisha.
Urusi
nayo ina mfumo wa kisasa zaidi wa kurusha makombora kutoka ardhini hadi
hewani katika kambi yake ya Syria lakini kwa sababu zisizoeleweka
hawajaweza kuzuia mashambulizi ya Waisraeli.
Kufuatia amri ya rais Donald Trump, meli mbili za kivita za Marekani
zimerusha makombora 59 ya kasi kutoka mashariki mwa bahari ya
Mediterenia katika kambi ya jeshi la anga la Syria mjini Homs.
Kulingana na Pentagon, walilenga ndege, majumba ya ndege na vituo vya mafuta, na maeneo ya kuweka silaha.
Maafisa wa Marekani wanadai kwamba waliviarifu vikosi vya Urusi kabla ya kutekeleza mashambulizi hayo ya makombora.
Rais
Trump alitangaza kuidhinisha shambulio hilo akiwa jimboni Florida
alipokuwa anakutana na rais wa China Xi Jinping, na alisema kuwa Rais
Assad ni dikteta huku akitaka jamii ya kimataifa kusaidia kumaliza vita
nchini Syria.
Vituo vya habari nchini Syria vimesema kuwa watu
tisa waliuawa kutokana na shambulizi hilo, wanne wakiwa watoto, lakini
BBC haijaweza kudhibitisha hayo.
Marekani imefanya mashambulizi
nchini Syria kuanzia mwaka wa 2014 lakini hii ni mara ya kwanza kulenga
kikosi cha serikali ya Assad.
Serikali ya Urusi ni mojawapo ya rafiki wa serikali ya Assad na vikosi vyake vimekuwa vikilenga makundi ya waasi kule Syria.
Rais
wa Urusi Vladmir Putin anaamini mashambulizi hayo katika kambi ya anga
ya Syria yamekiuka sheria za kimataifa na yamevuruga pakubwa mahusiano
kati ya Marekani na Urusi.
Moscow imetaja mashambulio hayo kama uchokozi mkali dhidi ya taifa huru.
Msemaji
wa rais Putin (Dmitry Peskov) amesema kwamba kando na kukiuka sheria za
kimataifa , Washington imesababisha uharibifu mkubwa katika uhusiano na
Moscow.
Wizara ya mambo ya nje imetangaza kusitishwa kwa
makubaliano na jeshi la Marekani yalioundwa kuzuia mashambulio ya anga
ya Syria.
chanzo:Bbc.
Comments