
Akizungumza na Mwanahabari wetu mtaalam wa masuala ya uchumi hapa
Zanzibar Dk.Mohammed Hafidh Khalfan ambae hivi karibuni ametunukiwa tuzo
ya mshauri bora wa masuala shariah na taasisi ya Alhuda Center of
Islamic banking and Economics iliopo Dubai.
Amesema kukosekana kwa kanuni hizo hivi sasa benki hizo zimekuwa
zikifanya kazi katika mazingira magumu kutokana kutegemea kanuni za
benki za kawaida.
Hata hivyo Dk.Mohammed amesema kinachokosekana hivi sasa kwa mashehe
hao ni kuweza kuunganisha taaluma zao kisharia walizozisoma na taratibu
za kifedha ili kuwa na mchango mzuri katika sekta hiyo.
Aidha ameitaka jamii kuzitumia ipasavyo benk za kiislam bila
kuzingatia itikadi zao za dini kwani benki hizo zipo kwa ajili ya kutoa
huduma kwa wananchi wote.
chanzo: Zanzibar24.
Comments