
Macron mwenye umri wa miaka thelathini na tisa na aliyewahi
kuwekeza katika sekta ya benki, hajawahi kuingia katika kinyang'anyiro
cha uchaguzi kabla, amesema, shaka, hofu na hamu ya mabadiliko
aliyokumbana nayo katika kampeni ndio iliyosababisha wapiga kura kuacha
vyama vikuu vya kisiasa ambavyo vimekuwepo uongozini kwa miaka
thelathini.
"Nimesikia katika miezi iliyopita na leo tena, shaka,
hasira na uoga waliokuwa nao wafaransa. Na hamu ya mabadiliko. Hiki
ndicho kilichowasukuma kuacha vyama vikuu viwili vilivyotawala kwa zaidi
ya miaka thelathini.")
Ameongeza kusema kazi yake hivi sasa ni
kuipatanisha nchi na kuunganisha nguvu kwa ajili ya duru ya pili ya
uchaguzi."wiki mbili kuanzia sasa, nataka niwe rais wenu. (CROWD
CHEERING) Rais wa raia wote wa ufaransa.
Kwa upande wake, Le Pen
ameyaelezea matokeo hayo kuwa ni ya kihistoria. Huku akijiita kuwa yeye
ni ndio chaguo la wafaransa na kusema kuwa muda umefika wa kuwabadilisha
watu.
"Wakati umefika wa kuwaweka huru raia wa ufaransa na jamii
yote wa rais wa Ufaransa bila kusahau marafiki zetu walio nje ambao
wameniamini na naona fahari kwa imani walioonyesha kwangu.")
Rais wa ufaransa amempigia simu bwana Macron na kumpongeza, bila kuonyesha kumuunga mkono rasmi.
Mmoja wa wasaidizi amesema haikuna vigumu kujua
chaguo lake kati ya waziri aliyefanya kazi nae na mwakilishi mwenye
mrengo wa kulia.
Francois Fillon ambae ni mgombea wa mrengo wa
kati, na aliyewahi kuwa waziri mkuu, ambae pia aliwahi kukabiliwa na
tuhuma za ufisadi, wakati akiwahutubia wafuasi wake amesema atampigia
kura Macron.
Wakati hayo yakijiri, kumetokea vurugu katikati mwa
jiji la Paris zilizohusisha vijana wenye mrengo wa kushoto ambao
hawakufurahishwa na ushindi wa Le Pen.
Polisi walipambana nao kwa kuwapiga viboko.Vile vile kumekuwa na maandamano magharibi mwa mji wa Nantes.
Tayari viongozi mbali mbali wa nchi za ulaya wameanza kuonyesha kumuunga mkono Macron.
Msemaji wa Chancellor wa ujerumani Angela Merkel amemtakia kila la heri, na kusifu msimamo wake kuunga mkono Umoja wa Ulaya.

chanzo:Bbc.
Comments