
Imeelezwa kuwa hali ya uelewa wa somo la lugha ya Kiingereza ktk
shule za msingi imedhihirika kuwa mbaya sana hasa kwa shule za Serikali.
52% ya wanafunzi wa darasa la 7 hawawezi kusoma hadithi ya kiingereza
ya darasa la 2. Vilevile 13% tu ya wanafunzi wa darasa la 3 ndio
walioweza kusoma hadithi hiyo.
Hii ilikuwa ni moja ya matokeo ya utafiti wa taasisi ya TWAWEZA
wakishirikiana na Uwezo Tanzania wakifanya Tathmini ya matokeo ya
kujifunza nchini.

Je hii inachangia ufaulu mbaya wa wanafunzi kidato cha nne?
chanzo: zanzibar24.
Comments