
Marekani na mataifa mengine ya magharibi yamemshutumu Rais wa Syria,
Bashar Assad na serikali yake kwa kile walichodai shambulio la kutumia
silaha za kemikali la siku ya jumanne mjini Khan Sheikhoun.
Trump amesema vifo vya watoto vimebadili mtazamo wake kwa Assad.

Marekani, Uingereza na Ufaransa, zote zimemshutumu
mshirika wa Serikali ya Syria kwa kile kilichotoka katika mji wa Khan
Sheikhoun.
Waziri
wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson ambaye anatarajiwa kufanya
ziara mjini Moscow nchini Urusi juma lijalo, ameitaka Urusi ifikiri kwa
makini kuhusu uhusiano wake na Syria.
hakuna shaka yeyote kuwa utawala wa Syria chini ya Bashar Al Assad
unahusika na shambulio hili la kinyama na tunaona sasa ni wasaa kwa
warusi kufikiri kwa makinni kwelikweli kuhusu kuendelea kuunga mkono
utawala wa Assad''

chanzo:Bbc.
Comments