
Tanzania imeiomba serikali ya Kenya kupuuzilia mbali taarifa hizo na
badala yake, nchi hizo mbili "ziangazie kuimarisha ushirikiano wa
kidiplomasia na kibiashara ambao umekuwepo."
Taarifa hizo zilisababisha maandamano na vurugu katika mji huo mapema wiki hii, Wakenya wakilalamika.
Shughuli za kiserikali na za kibiashara katika mji huo zilitatizwa na vurugu hizo, sana Jumatatu.
Katibu
katika wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa jumuiya ya Afrika
Mashariki Dkt Aziz Mlima amesema taarifa hizo ni za uongo.
Alisema
lengo la taarifa hizo ni "kumharibia Rais Magufuli sifa zake nzuri
ambazo amejizolea kufikia sasa pamoja na picha nzuri ya Tanzania kwa
jumla."
Dkt Aziz hata hivyoa amesema sheria za uhamiaji ni sharti zifuatwe.

Comments