Tanzania kuiga wa Korea.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January MakambaSERIKALI imesema itaiga mpango wa Korea wa utunzaji mazingira kwa njia za asili (Green Growth) kwa maendeleo endelevu, ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira wakati nchi inapoelekea katika uchumi wa viwanda.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nne wa mpango huo ulioandaliwa na Korea na Benki ya Dunia.


January alisema pamoja na Korea kuwa na maendeleo makubwa ya viwanda, lakini imekabiliana na uharibifu wa mazingira kupitia mpango huo na kupunguza hewa ukaa.

Alisema katika kuelekea uchumi wa viwanda ndani ya miaka 10 ijayo, nchi inaweza kuwa mstari wa mbele katika kuleta ‘Green Growth’ kupitia mikakati bora na sera ya rasilimali.
 chanzo:Habarileo.

Comments