Kwa mujibu wa Mkuu wa Takukuru Mkoa, Holle Makungu, washtakiwa
wengine waliofikishwa mahakamani ni Magera Andrew (40), Ofisa Kilimo
Msaidizi halmashauri hiyo na Pilly Mzita (53) ambaye alikuwa karani wa
mahesabu katika Halmashauri ya Musoma na sasa yuko halmashauri ya
Butiama.
Washtakiwa wamefikishwa mahakamani jana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa
Mahakama ya Wilaya Musoma na kusomewa mashtaka na waendesha mashtaka wa
Takukuru, William Fussi akisaidiana na Moses Malewo.
Katika mashitaka ya kwanza, upande wa mashtaka umedai kuwa Septemba
1, 2009, Andrew alitumia vibaya mamlaka yake kwa kuiwezesha Kampuni ya
Winam General Traders kulipwa Sh 16,800,000 kinyume cha mkataba wa
ukarabati wa lambo la Kisamwene.
Katika mashitaka ya pili upande wa mashtaka umedai kuwa Aprili 1,
2009, Andrew alitumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri wake kwamba
Hemed Maftah alistahili kulipwa Sh 640,000 kwa huduma ya uhakiki na
upimaji malambo Wilaya ya Musoma.
Katika mashitaka ya tatu upande wa mashtaka umedai kuwa Aprili 24,
2009 kuwa Kunei alitumia nyaraka za uongo kuonesha kuwa Wakala wa
Uchimbaji Visima na Mabwawa, Maftah aliipa ushauri Halmashauri ya
Musoma.
Katika mashitaka ya nne upande wa mashtaka umedai kuwa Septemba 11,
2009 kwa lengo la kumdanganya mwajiri Mzita aliandaa hundi ya malipo Sh
640,000 kwa wakala wa uchimbaji visima na mabwawa, Maftah.
Katika mashitaka ya tano upande wa mashtaka umedai kuwa Novemba, 2009
katika tarehe zisizofahamika Andrew akiwa na nia ovu ya kudanganya
alifoji sahihi ya Maftah kuonesha ndiye aliyeandaa fomu ya kukamilisha
mradi.
Mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Kunei amekana shtaka dhidi yake na washtakiwa wengine wawili hawakuwepo mahakamani.
Upande wa mashtaka umeiarifu mahakama kuwa uchunguzi wa shauri
umekamilika na umeomba tarehe nyingine ya kutaja shauri kwa kuwa
washtakiwa wengine hawakufika mahakamani na haukuwa na pingamizi dhidi
ya dhamana ya mshtakiwa.
Kesi imeahirishwa hadi Aprili 28, mwaka huu itakapokuja kwa kutajwa
na mshtakiwa yuko nje kwa dhamana ambapo amewasilisha hati ya nyumba
yenye thamani isiyopungua Sh milioni 2.7 pamoja na wadhamini wawili
waliosaini dhamana ya Sh milioni 2.4 kila mmoja.
chanzo:Habarileo.
Comments