Spika wa Bunge Aagiza Polisi kumkamata Mbunge Halima Mdee......Mbowe nae Katakiwa Kufika Kamati ya Maadili Kujieleza.
Spika
wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameliagiza
Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe (CHADEMA)
Halima Mdee kujibu tuhuma za kutoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa
uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4,
2017.
Pia
Mbunge Freeman Mbowe ameagizwa na Spika Ndugai kufika mbele ya Kamati
ya Maadili leo akituhumiwa kutukana bunge kufuatia uchaguzi huo wa
EALA.
Mwingine anayetarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Kinga, Maadili na Madaraka leo ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Pastory Mnyeti ambaye ameitwa na kamati hiyo na anatakiwa kufika leo.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments