Simba yamalizana na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.

simbaSimba imetangaza kuwa tayari imelipa kodi iliyokuwa inadaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kuingiza nyasi bandia nchini ambazo zilikuwa zimeletwa kwa ajili ya kuwekwa katika uwanja wa Simba uliopo Bunju Dar es Salam.

Katika taarifa ambayo imetolewa na Simba SC kupitia akaunti yake ya Instagram imesema tayari imelipa kodi na nyasi hizo kwa sasa zitapelekwa Bunju kwa ajili ya kuwekwa katika uwanja ambao itakuwa inautumia kufanya mazoezi.


Taarifa Rasmi kuhusiana na Nyasi Bandia, Mpaka sasa Tumeshalipia Kodi yote ya Nyasi Bandia, Kinachoendelea sasa ivi ni Wakala wetu kumalizia taratibu za Kutoa Container zenye nyasi hizo bandarini kwenda kuwekwa rasmi katika uwanja wetu wa Bunju.
chanzo:zanzibar24.

Comments