Serikali
ya Tanzania na Uganda zimesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano
(BASA), katika usafiri wa anga utakaowezesha nchi hizo kutoa huduma bora
za anga na kufungua fursa za kibiashara kwa wananchi wake.
Akizungumza
mara baada ya kusaini mkataba huo jijini Arusha, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema mkataba huo
utaruhusu ndege za nchi hizo mbili kutua na kuruka bila vikwazo vyovyote
katika nchi hizo.
"Naamini
ushirikiano huu utaboresha huduma zinazotolewa na Mamlaka za usafiri wa
Anga na hivyo kuongeza viwango vya usalama wa usafiri huu", amasesema Prof. Mbarawa.
Naye
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa, amesisitiza kuwa mkataba
huo ni muendelezo wa ushirikiano mwema baina ya Tanzania na Uganda na
hivyo kuchochea maendeleo ya uchumi kwa raia wa nchi hizo.
Ushirikiano
wa Tanzania na Uganda ni sehemu ya mkakati wa nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki katika kuwezesha wananchi wake kunufaika na fursa za kijamii,
kiuchumi, kiusalama na kiutamaduni.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments