
Akizungumza katika kikao kilichowakutanisha wamiliki wa vyombo vya
habari, watendaji wakuu wa vyombo hivyo na wajumbe wa kamati ya
maendeleo ya wanawake habari na utali ya baraza la wawakilishi Zanzibar
Mwenyekiti wa kamati hiyo Ally Suleiman Shihata amesema ili kuimarisha
maendeleo zaidi ni vyema kwa vyombo hivyo kufuata sheria za nchi
zilizopo.
Kwa upande wao Baadhi ya wamiliki wa vyombo hivyo wamesema utozwaji
wa kodi za kulipia minara ya kurushia matangazo, kutopewa uhuru wa
nafasi za kurusha matangazo ya moja kwa moja kutoka katika matukio ya
kitaifa na viongozi kutotoa mashirikiano mazuri kati yao ni miongoni mwa
matatizo yanayokwamisha maendeleo ya habari.
Nae waziri wa habari utalii utamaduni na michezo
Rashid Ally Juma,amesema mkutano huo umeongeza mwamko wa ushirikiano
baina ya vyombo vya habari na serikali katika kuihudumia jamii na
kuongeza kasi ya upatikanaji wa taarifa .
chanzo:Zanzibar24.
Comments