Serikali kuanzisha bima ya afya kwa wazee Nchini.

Katibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga amesema Serikali  inakusudia kusajili wazee wote nchini ili waingizwe kwenye mfumo wa kupata huduma bora ya afya kwa njia ya Bima ya Afya.

Katibu Nkinga alisema hayo mjini Dodoma kwamba wizara imekamilisha kufanyia kazi muswada huo wa kuwasaidia wazee.

Amesema Serikali ieamua kufanya ili kuhakikisha kuwa wazee wote wanapatiwa huduma hiyo hiyo ili kuwawezesha kuwapatia matibabu kwa urahisi ambo ambalo lilikuwa likiwapa usumbufu.
“Tunatafanyia kazi suala hilo ili kuhakikisha wazee wote wanasajiliwa na kupata huduma ya afya, jambo ambalo limekuwa likiwasumbua wazee katika kupata huduma hizo za afya kwa muda mrefu,” alisema
“Wizara hiyo imeandaa muswada huo ambao upo kwenye hatua muhimu ya uamuzi, ambao umechelewa kukamilika, lakini hata hivyo utakamilika karibuni,” alisema.
Kiongozi wa Wazee hao, Wakili Clotilda Kokupima (80), alieleza kwa masikitiko kwamba kitendo cha serikali kuchelewesha sheria ya wazee hao kunawafanya wasiwe na furaha kwani sasa ni miaka 10 tangu muswada huo umeanza kuandaliwa hadi leo na hujawa sheria.
Kokupima anayefanya kazi ya kusaidia wazee hao kisheria nchini, alisema muswada huo umekuwa ukiandikwa kwa zaidi ya miaka 10 hadi sasa na haujakamilika na sijui ni lini utakamilika.
“Muswada huo haujatajwa katika bunge linaloendelea kama mkutano uliandaliwa na Shirika la Kimataifa la HelpAge ambao uliwakutanisha wakurugenzi wa hospitali za rufaa, za mikoa na za wilaya na maofisa waandamizi kutoka wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ulivyoagiza ufikishwe,” alisema.
chanzo:zanzibar24.

Comments