
Waziri Ummy Mwalimu aliyasema hayo katika mahojiano maalumu mjini
hapa kuwa mchakato huo ungefikia asilimia 100 jana kukamilika kwake.
“Kimsingi hapa tunachokifanya ni kufanya majumuisho tu ya mchakato
mzima ili sasa nitoe tamko la ni madaktari wangapi na wenye sifa zipi
wamepatikana ili kwenda Kenya kutoa huduma za afya.
“Nadhani hadi jioni
leo (jana) kazi hii itakuwa imekamilika na hivyo naamini kesho tutatoa
tamko letu rasmi juu ya mchakato huu mzima,” alisema.
Aitha amesema, Tanzania ilikubali ombi la kuipatia Kenya madaktari
500 watakaoisaidia nchi hiyo kukabiliana na tatizo la uhaba wa madaktari
katika vituo vyake vya tiba hasa baada ya kutokea kwa mgomo wa
madaktari nchini humo hivi karibuni.
Rais John Magufuli alikubali kutoa madaktari hao Machi 18, mwaka huu
Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya kufanya mazungumzo na ujumbe wa
viongozi wa Wizara ya Afya ya Kenya uliotumwa na Rais wa nchi hiyo,
Uhuru Kenyatta.
chanzo:zanzibar24.
Comments