
Hatua hiyo imekuja mara baada ya kushindwa kufikia maamuzi, mazungunzo yaliyokuwa yakiongozwa na maaskofu wa kanisa katoliki.
Mpaka
sasa chama tawala na upinzani wameshindwa kuafikiana kuhusu uteuzi wa
waziri mkuu ,Mazungumzo haya mapya wanatarajia jibu la rais Joseph
Kabila kwa maskofu wa kanisa katoliki ambao walijaribu kupatanisha
wanasiasa wa upinzani na wa chama tawala kwa muda wa miezi mitatu
lakini jitihada zao zilishindikana.
Hata hivyo kufuatana na
msimamo wa kila upande , wakishindwa kuafikiana kuhusu kuteuliwa kwa
waziri mkuu mpya ambae alipaswa kutoka upande wa upinzani baada ya
kushindwa maskofu waliomba rais Joseph Kabila kujaribu mwenyewe
kutautua mgororo huu lakini hadi sasa vyama vikuu vya upinzani
vimemsusia rais huyo na kukataa kufanya uchaguzi .
Mjadala huu
mpya unaweza kuchukua muda wa siku tatu na hapo baadae rais Kabila
atatoa hotuba ya mwisho bungeni juu ya mgororo huo wa kisisisa.
Kwa
sasa maeneo mengi ya nchi hiyo yako kwenye hali ya wasiwasi, huku
baadhi ya shughuli mbalimbali mjini Kinshasa kusimama kama vile kufungwa
kwa baadhi ya maduka,shule na baadhi ya ofisi .
chanzo:Bbc.
Comments