Taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari Maelezo inaeleza kuwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Rabikira Mushi alikabishi zawadi hizo kwa niaba ya Rais.
Mushi alisema utoaji wa zawadi hizi umekuwa ni utaratibu wa kawaida kwa Rais Magufuli ambapo alitoa zawadi za vyakula kama vile mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ili kuwawezesha makundi yenye mahitaji maalum kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengine.
Baadhi ya vituo vilivyofaidika na zawaidi hizo kwa mkoa wa Dar es Salaam na Zanzibar ni,Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini,Makao ya Watoto Mburahati,Makao ya Watoto Msimbazi.Makao ya Watoto Kijiji cha Furaha,Makao ya Watoto SOS Children’s Village Tanzania.
Comments