
Wakati wa utawala wake wa miaka ishirini na miwili , Rais Jammeh
mara kwa mara alilipuuza bunge , na kupitisha sheria zake bila kupata
ushauri wowote.
Chini ya rais mpya Adama Barrow, matarajio ni makubwa kwamba bunge la taifa litakuwa na jukumu muhimu la kutunga sheria .
Baraza la mawaziri la Bwana Barrow linajumuisha wakuu wa vyama saba
tofauti vya kisiasa ambao waligombea katika uchaguzi uliopita .

chanzo:Bbc.
Comments