Polisi wawapiga risasi na kuwaua mifugo wengi Kenya.

Polisi wawaua mifugo wengi nchini Kenya kwa kuwapiga risasiRipoti ya kutoa kituo cha televisheni cha NTV cha nchini Kenya zinasema kuwa maafisa wa usalama waliotumwa eneo la Laikipia kufuatia uvamizi ulitokea katika mashamba ya kibinafsi na mahoteli uliofanya na wafugaji, wamekuwa wakiwaua kwa kuwapiga risasi mifugo wanaomilikiwa na jamii za wafugaji.

Awali mamlaka zilikana madai kuwa polisi wamekuwa wakiwaua mifugo kulipiza uvamizi wa wafugaji hao.
Ukame unaoendelea kushuhudiwa unaripotiwa kuwalazimu wafugaji kutafuta malisho kwenye mashamba ya kibinafsi, lakini baadhi yao wameripotiwa kupora na kuchoma moto hoteli za kibinafsi.
Ukame unaendelea kushuhudiwa unaripotiwa kuwalazimu wafugaji kutafuta malisho kwenye mashamba ya kibinafsiMmoja wa wafugaji aliyehojiwa alisema kuwa polisi waliwaua mifugo wake kwa kuwapiga risasi.
chanzo:Bbc.

Comments