
Mzazi huyo aliyatambulika kwa jina la Asma Juma, anawatuhumu wauguzi
wa hospitali hiyo kumuiba mtoto wake mmoja kwa kudai, awali wakati
alipokuwa na ujauzito picha za Ultrasound alizowahi kupima zilionyesha
kuwa ana ujauzito wa mapacha na hata alipokuwa hospitalini hapo
alimsikia nesi aliyekuwa akimuhudumia akithibitisha kua ana watoto
wawili.
Asma alisema “Wakati nipo chumba cha upasuaji, baada ya kuambiwa
nafanyiwa operesheni, yule nesi aliyekuwa ananihudumia akiwa na mtu
mwingine nilimsikia akisema ‘viko viwili’ akimaanisha wako watoto
wawili, yule nesi aliniambia nisijitingishe, baadaye walinichoma sindano
nikapoteza fahamu.”
“Nilivyozinduka nikajikuta nipo chumba cha pili nikiwa nasikia
maumivu makali sana, niliwaomba dawa wakaniambia nitazikuta wodini hapo
hakuna dawa za maumivu. Nilifanyiwa operesheni saa nane hadi saa kumi na
mbili ndipo nikapelekwa wodini, kwa muda wote huo sikupewa watoto
wangu.
Nimeletewa mtoto mmoja saa kumi na moja alfajiri nakumbuka wakati
nipo wodini nilimsikia yule nesi aliyekuwa akinihudumia akisema
‘Ultrasound’ zinadanganya. Ilisema ana watoto wawili kumbe ni mmoja.
Kwakweli hadi sasa sielewi,” ameongeza.
chanzo: zanzibar24.
Comments