Hayo yalibainishwa Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo kwa niaba ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu
Hassan wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Nishati kupitia Mradi wa Tanzania
na Uholanzi wa Masuala ya Nishati (TDECB).
Profesa Muhongo alisema jukwaa hilo linalenga kutoa mchango katika
sekta za nishati mbadala na gesi kupitia tafiti zenye viwango, wataalamu
na kusaidia katika sera ya nchi kuhusu masuala hayo.
Alisema vyuo ambavyo vimelengwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Taasisi ya Sayansi na
Teknolojia ya Karume Zanzibar pamoja na vyuo vitatu kutoka nchini
Uholanzi.
Alisema vyuo hivyo vitawezeshwa kupata vitendea kazi, mafunzo kuhusu nishati na watasaidiwa katika masuala ya sera.
Alieleza kuwa barani Afrika watu wasiopata nishati ni asilimia 46, na
kwa nchini, vijijini watu wenye fursa hiyo ya kupata nishati ni
asilimia 49.5, Tanzania nzima inapata umeme kwa asilimia 67.5 huku
katika miji yote ni asilimia 97.5 hiyo ni kutokana na takwimu za Desemba
mwaka jana.
Kwa upande wake, Naibu Makamu Mkuu wa Udsm, Profesa Florens Lugano
alisema malengo ya jukwaa hilo ni kufikisha Tanzania kukuza uchumi wa
viwanda, kutengeneza nafasi za ajira na kuboresha maisha ya Watanzania
kwa ujumla.
Profesa Lugano alisema pamoja na changamoto nyingi zinazoikabili
sekta hiyo, sera zilizopo zimesaidia kuleta mafanikio makubwa
yanayoonekana.
Comments