Mtuhumiwa wa Richmond huru.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Naeem Fire baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.
Akitoa uamuzi, Hakimu Mfawidhi,Cyprian Mkeha alimuachia huru jana Gire baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka mawili ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo.
Uamuzi huo ni wa pili kutolewa na mahakama hiyo dhidi ya mashtaka yaliyokuwa yakimkabili Gire.
chanzo:Mwananchi.

Comments