
Mtuhumiwa huyo alichupa katika gari ya polisi wakati iliposimama nje
ya mahakama ya Mkoa Chake Chake alipofikishwa leo asubuhi kwa ajili ya
kwenda kujibu kesi hiyo inayomkabili.
Mtuhumiwa huyo na wenzake watano wanatuhumiwa kufanya wizi wa fedha
riali 250 sawa na milioni mbili za kitanzania pamoja na vito mbali mbali
vya mapambo ikiwemo mikufu, pete na vitu vyengine vyenye thamani ya
zaidi ya shilingi milioni 3, mali ya Moza Hilal Shamis mkaazi Kichaka
Mtangani Mkoani Pemba .
Imedaiwa mahakamani hapo Mtuhumiwa Mohammed Mwalim Ali, na wenzake
Saleh Juma Muhene , Othaman Awesu Bakar, Khalfan Mwalim Khalfan(Fangasi,
Khamis Juma Hemed, kinyume cha Sheria walitenda kosa la uvamizi na
kuiba, huku Bi Mgeni Amour Kombo (32) akituhumiwa kupokea mali za wizi.
Hakim wa Mahakama ya Mkoa Chake Chake Khamis Ali Simai ameagiza
kutafutwa na kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kufikishwa mbele ya
mahakama hiyo, huku washitakiwa namba 3 na 4 Othman Awesu Bakar na
Khalfan Mwalim Khalfan wakirejeshwa rumande hadi April 27 mwaka huu,
wengi watatu wamepatiwa dhamana.
Chanzo:Zanzibar24.
Comments