
Kauli hiyo
imetolewa na Afisa Mipango wa wilaya ya Chakechake Kassim Juma,
alipokuwa akizungumza kwenye mafunzo ya utayarishaji wa vitalu bora
yalioandalia na Jumuia ya Mazingira Vitongoji VECA na kufanyika skuli ya
maandalizi Madungu Chakechake.
Alisema vyandarua
vinayotolewa na serikali ni kwa ajili ya kinga ya mbua wanaosababisha
malaria, na sio kutumika kwenye kukinga wadudu wanaoharibu miche.
Alisema VECA aipo
kwa ajili ya kutoa elimu hiyo, hivyo ni vyema wanaoatika miche na wenye
malengo ya kufanya hivyo, wasisite kuitumia jumuia hiyo ili wapate
taaluma ya kina.
Aidha Afisa
mipango huyo, alisema moja ya kosa linalofanywa na wanaotika miche
kwenye vitalu ni kufanya kazi hiyo zaidi kwa ajili ya kujipatia kipato
badala ya kuwa na lengo la kuhifadhi mazingira.
“Kila mkulima
anaesimama hapa anasema anatumia chandarua kwa ajili ya kuhifadhia
miche, hiyo sio njia sahihi maana hivyo ni kwa ajili ya wananchi
kujikinga na mbu wanaosababisha malaria hivyo acheni utamaduni
huo’’,alifafanua.
Katika hatua
nyengine Afisa mipango huyo amepongeza VECA kwa jitihada zake za
makusudi katika kuwapa taaluma wananchi wakiwemo wa upandaji miti na
wanaoatika vitalu.
Mapema akifungua
mafunzo hayo ya siku tatu, Katibu wa VECA Sifuni Ali Haji aliwataka
waatika miche hao kuhakikisha mafunzo walioyapata wanawapa na wenzao ili
lengo la VECA la kuhifadhi mazingira lifikiwe.
Hata hivyo Katibu
huyo alisema wanawake wanayonafasi kubwa ya kuwaelimisha wanaume kuacha
kuangusha miti bila ya kuwa na utaratibu wa kupanda mengine.
“Wanaume ndio
hasa wanaoongoza kwa kukata miti iwe ni kwa ajili ya kupiga mkaa,
ujenzi, kuni au kutengenezea fanicha, sasa sisi wanawake lazima hili
tulikemee, maana waathirika wakubwa ni sisi’’,alifafanua.
Akiwasilisha njia
sahihi ya utayarishaji wa vitalu, mtoa mada Mohamed Najim Omar, alisema
suala la chanzo cha maji, usawa na eneo ni miongoni mwa mambo ya
kuzingatia kwa muatikaji wa miche.
Baashi ya
washiriki wa mafunzo hayo, wamesema laiti kama VECA ingepata ufadhili
zamani na kuwapa mafunzo hayo, wengekuwa wameshapiha hatua kubwa ya
kuhifadhi mazingira.
Mafunzo hayo ya
siku tatu, ambayo yametayarishwa na Jumuia ya Maendeleo Vitongoji ‘VECA’
na kufadhiliwa na Shirika la Uhifadhi wa kimataifa la ‘Global green
grant fund’ la Marekani kupitia mfuko wa kimazingira wa duinia, mada
kadhaa zilijadiliwa ikiwa ni pamoja na wanawake na mazingira,
utayarishaji wa vitalu na athari za kutohifadhi mazingira.
chanzo:
Comments