
Polisi walimfuata kwa kasi mwanamuziki hiyo ambaya baadaye alisema
kuwa alikimbia kumsaidia rafiki yake kujifungua mtoto katika fukwe za
bahari.
Alikuwa na bili ya zaidi ya dola 450.
Terry Peck ambaye amefunguliwa mashtaka ya wizi baadaye alidai kuwa chakula hicho hakikua kimepikwa kwa njia inayotakikana.
Mwanamuziki
huyo mwenye umri wa miaka 33 alifikishwa mahakani leo Jumatatu baada ya
kisa hicho kilichotokea katika mgahawa wa Omeros Bros.
Australia si nchi pekee ambapo kuna visa vya wateja kula kwenye mikahawa na kukosa kulipa.
Mwezi
uliopita polisi wa Uhispania walimkamata mtu anayeshukiwa kuwa
kiongozi wa genge ambalo lilikuwa na tabia ya kula kwenye mikahawa na
kisha kutoroka kaskazini mwa nchi.

chanzo:Bbc.
Comments