
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo
kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi kamishna msaidizi muandamizi
wa polisi Hassan Nassirr Ali amesema kuwa kitendo alichofanya dereva
huyo kukimbia baada ya ajali hiyo kutokea si cha kiungwana kusema kuwa
watafanya upelelezi kuhakikisha wanamtia mikononi.
Mwili wa marehemu huyo ulipelekwa
hospitali ya mnazi mmoja kwa uchunguzi uliofanywa na mganga mkuu wa
hospitali hiyo na kuonesha kuwa ameumia kwa ndani ya moyo jambo ambalo
lilipeleka kupoteza maisha.
chanzo: zanzibar24.
Comments