
Wamesema jina lake ni Kim Sang-duk, lakini pia amekuwa akifahamika kamaTony Kim.
Mhadhiri
huyo ambaye ni Mmarekani wa asili ya Korea amekuwa akifunza katika Chuo
Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Pyongyang (PUST) kwa wiki kadha
kabla ya kukamatwa kwake.
Chuo kikuu hicho hata hivyo kimesema masuala yaliyopelekea kukamatwa kwa Bw Kim hayana uhusiano wowote na chuo hicho.
Bw Kim alikamatwa alipokuwa anajiandaa kuondoka Pyongyang.
Maafisa wa Korea Kaskazini bado hawajasema sababu iliyochangia kukamatwa kwake.
Shirika
la habari la Korea Kusini Yonhap limesema Bw Kim, ambaye umri wake ni
miaka hamsini hivi, alikuwa anashiriki katika mipango ya kutoa misaada
na alikuwa Korea Kaskazini kufanya mashauriano kuhusu juhudi za kusaidia
watu wasiojiweza.
Shirika hilo limesema Bw Kim aliwahi kuwa profesa katika chuo kikuu cha Yanbian nchini China.
Chansela
wa chuo kikuu cha PUST, Park Chan-mo, amenukuliwa na shirika la habari
la Reuters akisema Bw Kim "alikuwa anajihusisha na shughuli nyingine nje
ya PUST kama vile kusaidia kituo cha mayatima."
Bw
Kim amezuiliwa kipindi ambacho wasiwasi umekuwa ukiongezeka katika rasi
ya Korea huku meli za kivita za Marekani zikielekea eneo hilo.
Korea Kaskazini imetishia kuzishambulia meli hizo.
Marekani kwa muda imekuwa ikiituhumu Korea Kaskazini kwa kuwakamata na kuwazilia raia wake kisha kuwatumia kama rehani.
Bw Kim sasa ni raia wa tatu Mmarekani kuzuiliwa na Korea Kaskazini.
Mwezi
Aprili mwaka jana, Kim Dong-chul, 62, raia wa Marekani aliyezaliwa
Korea Kusini, alihukumiwa kifungo cha miaka 10 na kazi ngumu baada ya
kupatikana na makosa ya kufanya ujasusi nchini humo.
Alikuwa amekamatwa Oktoba mwaka uliotanguliwa.
Mwanafunzi
Mmarekani Otto Warmbier, 21, naye alikamatwa Januari mwaka jana
akijaribu kuiba bango la propaganda hotelini alipokuwa ziarani Korea
Kaskazini.
Alihukumiwa kufungwa jela miaka 15 na kazi ngumu kwa makosa ya uhalifu dhidi ya dola Machi mwaka 2016.
chanzo:Bbc.
Comments