Mlipuko wa bomu wauwa watu 15 Somalia.

Watu 15 wameuawa Nchini Somalia  kufuatia mlipuko wa Bomu lililokuwa limetegeshwa katika gari nje ya kambi ya jeshi katika mji Mogadishu.
Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Al Shabaab limekiri kufanya shambulio hilo ambalo ni tukio la hivi karibuni katika kampeni za wapiganaji hao ambalo inaendelea kuhatarisha usalama wa nchi.

Shambulio hilo limeharibu magari na kujeruhi watu karibu na wizara ya ulinzi mjini Mogadishu.
Mlipuko huo ingawa ulilenga msafara wa maafisa wa ngazi za juu wa jeshi, lakini idadi kubwa ya waliojeruhiwa ni wananchi wa kawaida waliokuwa karibu kwenye gari.
chanzo:zanzibar24.

Comments