MKUU wa WAUGUZI: Uhaba wa Wauguzi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja ya changia kuongeza vifo.

mnaziMkuu wa Wauguzi katika kitengo cha hospitali ya Mnazi mmoja  Haji Nyonje Pandu amesema Uhaba wa wauguzi katika Hospital hiyo ni miongoni mwa matatizo ya yanayorejesha nyuma azma ya serikali katika kupunguza vifo vya kina mama na watoto wakati wa kujifungua.

Akizungumza katika mkutano uliowakutanisha Viongozi wakuu wa  Mashirika ya umoja wa mataifa UN nchini na Viongozi wa Hospitali ya mnazi mmoja kuangalia maendeleo na Matatizo yanayoikumba hospital hiyo amesema  mbali na kuimarisha kwa jengo la kina mama na watoto lakini wanashindwa kufikia malengo kutokana na kukabiliwa na tatizo la uhaba wa wauguzi.


Hata hivyo amesema katika kufikia lengo walilolikusudia jumla ya wauguzi mia mbili hamsini wanahitajika ili kupunguza tatizo hilo pamoja na kuweza kurahisisha huduma za wauguzi kwa kina mama wanao hitaji huduma  hizo wakati wa kujifungua.

Kwa upande wake Afisa kutoka Shirika la umoja wa kimataifa Batul Abdi amesema katika kupunguza matatizo yanayoikabili hospiatal hiyo ni vyema kwa Serikali ya Zanzibar kuandaa utaratibu wa kuajiri wafanyakazi  watakaoziba nafasi za wauguzi ili kupunguza vifo vya kina mama na watoto vinavyojitokeza mara kwa mara.

Wakati huo huo Daktari Mkuu wa Hospital ya Mnazi Mmmoja Zanzibar Dk.Nuofal Kassim Muhammed  amesema mbali na kuwepo kwa tatizo hilo ujio wa wageni hao umeonesha kuridhika kwa jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na serikali na uwongozi wa hospital hiyo kwa kufikia hatua ya kuweza kujitegemea katika utendaji wao wa kazi.

Kwa mujibu wa kauli ya mkutano huo jumla ya kina mama wapatao 40 wanajifungua kwa siku ambapo wanahudumiwa na wauguzi watatu jambo linalowanyima fursa ya kukosa huduma bora na kupelekea kuengezeka kwa vifo vya kina Mama na Watoto.
chanzo:Zanzibar24.

Comments