Watu
wasiofahamika wamevamia mkutano wa wanachama wa CUF upande unaomuunga
mkono, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.
Mkutano
huo uliokuwa ukifanyika katika Hoteli ya Vina, Mabibo, ulipangwa kuanza
leo saa tano asubuhi lakini kabla haujaanza watu waliovalia soksi
nyeusi usoni(mask) walivamia na kuanza kuwapiga wanachama wa CUF na
waandishi waliokuwa kwenye mkutano huo.
Mtu mmoja miongoni mwa waliovamia mkutano wa wanachama wa CUF ameshambuliwa na wananchi wakati akijaribu kutoroka.
Mtu
huyo, ambaye hajafahamika alikuwa akitoroka pamoja na wenzake katika
eneo hilo la Vina Hotel Mabibo mara baada ya kutekeleza uvamizi huo
katika mkutano wa wanachama wa CUF.
Watu hao waliovamia mkutano huo, walikuwa na bastola.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments