
Mtuhumiwa huyo ni mara yake ya tatu kukamatwa na maafisa wa TAKUKURU kwa kosa la kuwatapeli watu 13.
Mbali na matukio ya kuchukua fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 4 laki mbili na themanini na nne elfu kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wahitimu wa vyuo vikuu, Makale amesema mtu huyo pia amekuwa akitumia cheo hicho cha Mkurugenzi wa TAKUKURU mkoa kujipatia huduma ya bure zikiwemo za kunyoa kwenye saloon, kitoweo cha samaki kutoka kwa wafanyabiashara na sehemu nyingine nyingi zinazotoa huduma kwa jami.
chanzo:zanzibar24.
Comments