Misri yatangaza miezi mitatu ya hali ya hatari.

Viongozi wa dhehebu la Coptic wamesema tukio hilo halitawatenga na jamii ya waislamuRais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi ametangaza miezi mitatu ya hali ya hatari nchini kote, kufuatia shambulizi la bomu ambalo limeua zaidi ya watu 40 katika makanisa mawili ya Coptic.
Jeshi litapelekwa kusaidia polisi kulinda maeneo muhimu na vikosi vya usalama vitaruhusiwa kukamatwa bila kibali cha kukamatia.

Kufuatia tukio hilo, Rais Sisi pia ametangaza kuundwa kwa baraza litakalopambana na ugaidi na watu wenye itikadi kali.
Vikosi vya usalama vimepelekwa kwa wingi katika mji wa AlexandriaKundi la wanamgambo wa kiislamu la Islamic state limekiri kuendesha mashambulizi hayo.
Ahmed Abdel Hady ni muislamu ambae anasema kamwe shambulio hilo halitaweza kuwagawa Wamisri.
Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi amesema tukio hilo sio la kufumbiwa machoWaislamu na Wakristo kwa pamoja wameungana nchini humo kupinga shambulizi hilo.
chanzo:Bbc.

Comments