Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge alitoa kauli hiyo wakati
akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mufindi Kaskazini, Mahmoud
Mgimwa (CCM) aliyetaka kujua lini mradi wa umwagiliaji wa Ikweha,
utaanza kufanya kazi.
Lwenge alisema miradi mingi ya umwagiliaji ilikwama kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo zilizosababishwa na makandarasi.
“Miradi ya umwagiliaji maji, ilikwama kutokana na matatizo mbalimbali
yakiwamo ya udhaifu wa usimamizi japo fedha zilitengwa kuendesha miradi
hiyo,” alisema.
Alisema, pamoja na kufanya mapitio ya miradi hiyo, pia wizara yake
inafanya usanifu wa miradi mipya ya umwagiliaji nchini ili kuanzisha
miradi mingine mipya.
Akijibu swali la msingi la Mgimwa, Waziri Lwenge alisema mradi wa
umwagijiliaji wa Ikweha, serikali ilitekeleza kwa awamu mbili, ya kwanza
ilitumia sh milioni 435.9 na awamu ya pili ilitumia Sh milioni 370.7.
Lwenge alisema, baada ya kukamilika awamu hizo mbili kulikuwa na
upungufu uliobainika na ulitakiwa kurekebishwa ndani ya kipindi cha
matazamio cha miezi 12 kilichotarajiwa kukamilika Agosti mwaka jana.
“Kutokana na ucheleweshaji wa malipo kwa kazi alizozifanya mkandarasi
huyo, iisababisha ucheleweshaji wa marekebisho ya upungufu huo,”
alisema.
“Lakini Halmashauri ya wilaya ya mufindi na mkandarasi wamekubaliana
marekebisho ya mradi huo yaanze kufanyika Aprili, mwaka huu,” alisema.
chanzo:Habarileo.
Comments