Mgogoro wa CUF ni hujuma zinazofanywa na chama Tawala.

maaalim
Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema mgogoro wa CUF ni hujuma zinazofanywa na chama Tawala.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu mkuu huyo amesema hizo ni hujuma zinazopangwa na kuendeshwa na dola ili kuua upinzani nchini na kunyamazisha kila kauli inayothubutu kuikosoa Serikali.

Lengo la mkakati huu sio CUF bali ni kuua UKAWA na upinzani. Hujuma hizi zinaelekezwa kwa bunge, vyma vya siasa, na taasisi zinazosimamia haki, watumiaji mitandao ya kijamii, wasanii, vyombo vya habari na wanasiasa wanaothubutu kusimamia wanachokiamini.
Katika njama za kudhoofisha upinzania, Chama cha CUF wanamtumia Lipumba ambapo ⁠⁠⁠⁠alivamia vikao vya chama, alimtumia msajili wa vyama, alivamia ofisi za chama, alitengua viongozi wa chama wakati yeye si mwanachama.
Maalim Seif alisema kuwa lipumba alianza njama hizo alipo karibishwa ikulu na kuanza kuishawishi CUF kukubali marudio ya uchaguzi mkuu Mwaka 2015.
Njama hizi zimeanza wakati Lipumba alivyokaribishwa ikulu mwaka jana. Nyote mnakumbuka sinema ya Lipumba baada ya ziara yake ya ikulu. ⁠⁠⁠Alianza kwa kutushawishi kukubali kurudia uchaguzi wa Zanzibar eti nitaendelea kuwa Makamu wa Rais“alisema Maalim Seif.
chanzo:zanzibar24.

Comments