Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Machi, 2017 umeongeza hadi kufikia asilimia 6.4 kutoka asilimia 5.5 mwezi Februari 2017.
Hayo
yalibainishwa katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS) kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam naja.
Taarifa
hiyo ilieleza kuwa hali hiyo inamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei
za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Machi 2017 imeongezeka
ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi
wa Februari 2017.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 108.44 mwezi
Machi 2017 kutoka 101.93 mwezi Machi 2016.Mfumuko wa Bei wa bidhaa za
vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Machi 2017 umeongezeka hadi
asilimia 11.0 kutoka asilimia 8.7 ilivyokuwa mwezi Februari 2017.
Taarifa
hiyo imeonesha kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa Bei wa mwezi Machi 2017
kumechangiwa na kuongezeka kwa bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na
bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Machi 2017
zikilinganishwa na bei za mwezi Machi 2016.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments