
Wote waliokuwa kwenye meli hiyo wameokolewa.
Urusi awali
ilikuwa imethibitisha kwamba meli ya Liman, ambayo ni sehemu ya kundi la
meli za taifa hilo katika Bahari Nyeusi ilikuwa imepatwa na hitilafu na
kwamba juhudi za kuizuia kuzama zilikuwa zinaendelea.
Chanzo cha kugongana kwa meli hizo hakijabainika lakini kulikuwa na ukungu mwingi eneo hilo.
Meli hiyo ya kijasusi iligonga meli yenye bendera ya Togo ambayo
ilikuwa ikisafirisha mizigo, vyombo vya habari Uturuki vinasema.
Waziri
mkuu wa Uturuki Binali Yildirim amezungumza na mwenzake wa Urusi Dmitry
Medvedev, na kumueleza masikitiko na huzuni yake kutokana na ajali
hiyo, duru katika afisi ya waziri mkuu huyo wa Uturuki zimenukuliwa na
shirika la habari la Reuters.
Kundi la Meli za Urusi Bahari Nyeusi
(BSF) hupitia mlango wa bahari wa Bosphorus Strait kuelekea bahari ya
Mediterranean, ambapo hushiriki katika harakati za kijeshi Syria.
Meli hiyo ya Urusi ilikuwa na watu 78 ambao waliokolewa wote.

Haijabainika iwapo meli hiyo ilikuwa inaelekea mlango wa bahari wa Bosphorus wakati huo.
chanzo:Bbc.
Comments