Meli mpya ya kudhibiti uvuvi harama yawasili Zanzibar.


Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imesema itahakikisha inasimamia azma yake ya kudhibiti uvuvi haramu Bahari kuu ili kuweza kufaidika na uchumi unaotokana na mazao ya baharini.

Akizungumza mara baada ya kuwasili kwa meli ya doria hapa Zanzibar inayotoka Madagaska ambayo inaelekea  katika ukanda wa bahari kuu kwaajili ya doria  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya kusimamia Uvuvi haramu wa Bahari mkuu Hosea Gonza Mbilinyi amesema kutokana na hasara inayopatikana  wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanawadhibiti wavuvi harama katika ukanda wa bahari mkuu ikiwa lengo ni kupiga vita uvuvi haramu na uwepo wa meli hiyo itasaidia kupunguza uvuvi harama.
Hata hivyo amesema Tanzania inashirikia na nchi mbalimbali ikiwemo Madagaska, Komoro, Muzambique, Kenya, Morishaz, Msumbiji na Shelisheli kwa na lengo la kudhibiti uvuvi harama bahari kuu ambapo wamedhaminiwa chini ya ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya IOC.
Doria hiyo ya kudhibiti uvuvi haramu ulianza mwezi huu wanne tarehe 11 hadi tarehe 8 mwezi wa 5 ambapo kila nchi inachangia asilimia 20 hadi 30 za gharama za uwendeshaji wa zoezi hilo.
chanzo:Zanzibar24

Comments